“Nilianza ku’hustle na ndoto ya kuwa mwanamuziki 1999 lakini nikaja kutoboa 2009” - Diamond

Diamond amewahi nukuliwa akisema kwamba wakati mmoja alilazimika kuiba mkufu wa mamake ili kuuza kupata pesa za kuruhusiwa kuingia kwenye ukumbi wa tamasha angalau kupata fursa ya kuonyesha kipaji chake.

Muhtasari

• Msanii huyo alisema kuwa wengi huenda wlaimjua kuanzia mwaka wa 2009 lakini hapo sipo safari yake ya muziki ilipoanzia.

• Mara kwa mara, msanii huyu hurudisha kumbukumbu nyuma jinsi maisha yalivyokuwa magumu akianza muziki na kulelewa na mama yake pekee.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: Maktaba

Msanii anayetajwa kuwa mtumbuizaji bora kuwahi kuonekana Afrika Mashariki, Diamond Platnumz amesimulia jinsi safari yake ya muziki ilivyoanza na ilikoanzia.

Akiwa na asili kutoka Kigoma, Magharibi mwa Tanzania, Diamond alijikokota kwa mwendo wa aste aste kisanaa hadi kuja kuipata nyota yake ya muziki jijini Dar es Salaam, jiji kuu la kibiashara la Tanzania, upande wa mashariki.

Akizungumzia historia yake kwenye jukwaa wakati anatumbuiza usiku wa Jumanne wakati wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru mkoani Tanga kwenye wilaya la Pangani, Diamond alisema kuwa hakulala na kuamka kujipata kileleni mwa moja ya wasanii marufu Zaidi Afrika.

Msanii huyo alisema kuwa wengi huenda wlaimjua kuanzia mwaka wa 2009 lakini hapo sipo safari yake ya muziki ilipoanzia.

Mkurugenzi mtendaji wa lebo ya WCB Wasafi na chombo cha habari cha Wasafi Media, alifichua kwamba alianza kuipambania ndoto yake ya kuwa mwanamuziki mwaka 1999 lakini akaja kutoboa tundu kimuziki miaka 10 baadae.

“Mimi nilianza Ku hustle na kupambania ndoto ya kuwa Mwanamuziki tangu mwaka 1999 lakini nilitoboa mwaka 2009, ni takribani miaka 10 baadae,” Diamond aliwaambia vijana wa Pangani.

Msanii huyo anayetajwa kuwa nambari mbili kwenye orodha ya wasanii Afrika Mashariki kwa mujibu wa orodha ya Forbes, aliwashauri vijana kutokufa moyo katika juhudi zai za kutafuta maisha, kwani mafanikio huchukua muda.

“Hivyo nawashauri vijana wenzangu tamaa ya kupambania ndoto zenu,” alishauri.

Kwa mujibu wa orodha ya Forbes ya mwaka jana, Diamond ana utajiri wa Zaidi ya bilioni 1.09 pesa za Kenya, nyuma ya msanii na mwanasiasa wa Uganda, Bobi Wine mwenye utajiri wa bilioni 1.2.

Mara kwa mara, msanii huyu hurudisha kumbukumbu nyuma jinsi maisha yalivyokuwa magumu akianza muziki na kulelewa na mama yake pekee.

Diamond amewahi nukuliwa akisema kwamba wakati mmoja alilazimika kuiba mkufu wa mamake ili kuuza kupata pesa za kuruhusiwa kuingia kwenye ukumbi wa tamasha angalau kupata fursa ya kuonyesha kipaji chake.