Ruto aendeleza kampeini dhidi ya BBI

Muhtasari
  • Hatuwezi angazia BBI peke yake William Ruto asema
  • Kwa miaka mingi tumekuwa tukiangazia kuwapa viongozi vyeo
William Ruto
Image: Hisani

Naibu rais William Ruto siku ya Jumapili alizuru eneo la Meru na kushikilia msimamo wake kupinga mchakato wa BBI.

Naibu rais alisema mjadala umekuwa kuhusu mamlaka na vyeo na sasa wakati umefika viongozi wazungumzie masuala yenye manufaa kwa wanananchi wa kawaida.

Huku akipinga mchakato wa BBI, Ruto alisema kuwa viongozi hawawezi angazia tu mfumo wa BBI.

"Hatuwezi kuangazia tu BBI ambayo lengo lake ni kuunda nafasi nne za kazi kwa watu ambao tayari wana kazi na tusahau kuhusu ajenda nne za serikali ambapo ujenzi wa nyumba ulikuwa utengeneze nafasi za kazi milioni nne." Alizungumza Ruto.

Ruto aliwataka viongozi wenzake waanze kuzungumzia hali ya wananchi na wala si mamlaka tu peke yake.

"Kwa miaka mingi tumekuwa tukizungumzia vyeo. Tumeongea kuhusu wadhifa wa waziri mkuu na manaibu wake na nyadhifa zingine kubwa. Ni wakati sasa mjadala uwe kuhusu vile tutabadilisha maisha ya mwananchi wa kawaida."

Viongozi walioandamana naye pia walipinga mchakato wa BBI.

(Mhariri Davis Ojiambo)