Vituko

Duh! Baba na mwanawe wamepikwa katika chungu kimoja!

Baada ya hafla ,huku mzee baba mtu na Grace wakiwa hawaangaliani ,kila mmoja kati yao hapo alijua kwamba uhusiano huo haungeenda popote .

Muhtasari
  •  Ilipangwa safari ya kwenda  Kerugoya alikozaliwa Geoff  na ambako babake alikuwa na biashara zake  licha ya kuwa mzee wake alikuwa akifanya kazi jijini na angesafiri kwenda na kurudi kutoka Kerugoya .
  • Siku ya siku ilipofika , Grace na jamaa zake walikaribishwa kwa akina Geoff ili mtoto wa kike awajue wazazi wa mume wake mtarajiwa

Mwanamke mmoja amesimulia mitandaoni jinsi mchezo wake wa kujaribu kula vya wanaume wawili tofauti akifikiri kwamba yeye ni stadi wa kuwakaganya alipojipata katika hali ya kutisha na hata akapatwa na woga wa kuendelea na mchezo huo wake .Grace    alikuwa na maisha ya kujihusisha na wanaume wengi kwa wakati mmoja huku kila mwanamme akijipatia majukumu katika maisha yake –kuanzia wa kumlipia kodi na yule ambaye alikuwa akimlipia karo katika  chuo kikuu .

 Lakini mtindo wake huo hatari wa maisha ulifika tamati wakati alipokutana na mpenzi wake wa sasa Geoff ambaye alikuwa  anamzidi umri kwa miaka mitano na akajiambia basi muda wake kuendelea na kuwahadaa wanaume kutumia mapenzi ulikuwa umekwisha na sasa anafaa kuanza kuzingatia uhusiano mmoja wa kudumu ili kujipata katika ndoa iwapo ingewezekana .

 Baada ya kujuana na Geoff kwa muda wa mwaka mmoja ,walianza kupifa mipango ya jinsi ya kutambulishana kwa familia zao kwa sababu wote kwa kauli moja walikuwa washaamua kwamba ndoa sasa ndio itakayokuwa  hatma yao kwa sababu walikuwa wamependana . Bila kujua kama  dunia ni ndogo sana na ni milima tu haikutani , Geoff ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtambulisha Grace kwa wazazi wake .

 

 Ilipangwa safari ya kwenda  Kerugoya alikozaliwa Geoff  na ambako babake alikuwa na biashara zake  licha ya kuwa mzee wake alikuwa akifanya kazi jijini na angesafiri kwenda na kurudi kutoka Kerugoya .

Siku ya siku ilipofika , Grace na jamaa zake walikaribishwa kwa akina Geoff ili mtoto wa kike awajue wazazi wa mume wake mtarajiwa

Ila mambo hayakuenda kama alivyofikiri kwa sababu walipofika ugenini , Grace alipatwa na mshutuko kumuona mzee ambaye alikuwa mpenzi wake wa hapo awali aliyekuwa akimlipia kodi ya nyumba mjini Nairobi! Babake Geoff wakati mmoja alikuwa sponsor wa Grace!

 Baba na mtoto hawakujua kwamba wamekula katika jungu moja na siku hiyo ndio iliyokuwa yao ya kwanza kuonana na hivyo basi Grace hakujua kwamba  angekutana na mazimwi ya vitendo vyake vya hapo awali .

 Baada ya hafla ,huku mzee  baba mtu na Grace wakiwa hawaangaliani ,kila mmoja kati yao hapo alijua kwamba uhusiano huo haungeenda popote .  Waliporudi mjini ,Grace bila kutoa notisi wala kusema lolote ,alibadilisha namabrai ya simu na kutokomea kabisa Geoff asijue kilichofanyika lakini msichana alikuwa ashafanya uamuzi wa kukatiza kabisa uhusiano ule .Angeishi vipi katika boma moja na baba na mwanawe ? Ingekuwa vipi iwapo mpenzi wake angegundua kwamba wakati mmoja babake alikuwa mpenzi wa   Mchumba wak? Aibu hizo zilikuwa  nzito sana kwa Grace kuendelea na uhusiano huo ili kungoja kushuhudia jambo ambalo lingetokea .