Mmiliki wa jengo lililoporomoka Ruaka akamatwa kwenye uwanja wa ndege wa JKIA

Alikamatwa katika angatua ya JKIA akiwa anaelekea Marekani.

Muhtasari

• Alipelekwa hospitali baada ya kulalamikia kuwa na shinikizo la damu.

• Jengo la Ruaka liliwaacha watu 3 wakiwa wamekufa. 

Pingu
Image: Radio Jambo

Mwanamume mmoja anayeaminika kuwa mmiliki wa jengo lililoporomoka eneo la Ruaka, Kiambu wiki jana alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa ya Jomo Kenyatta JKIA alipokuwa akijaribu kuondoka nchini.

Kulingana na ripoti ya Polisi mmiliki huyo wa jengo hio lililowaacha watu 3 wakiwa wameenda jongomeo ilisema mwanamume huyo alikuwa amefunga safari ya kuelekea Marekani.

Kulingana na mkuu wa idara ya kitengo cha kupambana na makosa ya jinai DCI ya Kaunti ya Kiambu Richard Mwaura alipokamatwa jamaa huyo alilalamika kuhusu shinikizo la damu lililofanya kikimbizwa hospitalini mara moja.

Kuporomoka kwa jengo hilo liliwaacha maafisa wa usalama kumwekea uangalizi mkali hadi atakapopata nafuu.

“Atashughulikiwa na kufikishwa mahakamani mara atakapopata nafuu. Kwa sasa yuko hospitalini lakini chini ya uangalizi wa polisi,” alisema Mwaura huku walipanga kumfungulia mastaka wakiwa na wadao wengine kwa kusababisha vifo na uharibifu wa mali.

Visa vya kuporomoka kwa mijengo kwenye kaunti ya Kiambu vimeibua hisia nzito kwa raia huku baada ya jengo lingine kuporomoka Jumatatu Novemba 21, 2022.

Kuporomoka kwa jengo hilo lililofanya wakaazi 100 kuachwa bila makazi kulimfanya Gavana wa wa Kaunti hiyo Kimani Wamatangi kuahidi kuwatafuta wamiliki wa majengo haya na kuwafungulia mastaka ya kuhatarisha maisha ya watu.

Wamatangi kwa upande wake alisema serikali ya kaunti ikishirikiana na serikali kuu kujaribu kufanya ukanguzi wa mijengo kama iko salama kwa wakaazi kuishi humo.