Mama wa watoto 6 azaa mbuzi baada ya kubeba ujauzito wake wa saba kwa miezi 11

Baada ya ujauzito huo kwenda miezi 11, alijifungua mbuzi na kiumbe hicho kilikuwa hai na kilijaribu kuinuka kutembea kwa Zaidi ya dakika 30 kabla ya kufa.

Muhtasari

• Baada ya tukio hilo la ajabu, mumewe alimtoroka na wanawe 6, na maisha yake yakabadilika kabisa, kwani alimtuhumu kwa kufanya mapenzi na mbuzi.

• Lakini kisayansi, haiwezi tokea kwamba mtu aliyeshiriki mapenzi na mnyama ana uwezo wa kuzaa mnyama au mnyama kuzaa binadamu.

Mwanamke azaa mbuzi
Mwanamke azaa mbuzi
Image: sCREENGRAB

Mwanamke mmoja alizua kusanga hospitalini baada ya kujifungua mbuzi nchini Uganda.

Mwanamke huyo kwa jina moja tu, Alphonsine ambaye ni mama wa watoto 6 alikuwa amebeba ujauzito wake was aba ambao uliishia kwake kujifungua mtoto wa mbuzi badala ya binadamu.

Kituko hicho kilirekodiwa na madaktari na Zaidi ya watu 200 waliofurika hapo baada ya taarifa kuenezwa. Hiki kilikuwa kitendo cha ushirikina ambacho anaamini kiliharibu ndoa yake kabisa.

Kabla ya kujifungua mbuzi, Alphonsine alikuwa amejifungua watoto 6, wote waliozaliwa bila matatizo yoyote lakini wakati wa ujauzito wake wa 7, kitu cha ajabu kilitokea kwani alibeba ujauzito huo kwa miezi 11 kinyume na miezi 9 ya kawaida.

Baada ya ujauzito huo kwenda miezi 11, alijifungua mbuzi na kiumbe hicho kilikuwa hai na kilijaribu kuinuka kutembea kwa Zaidi ya dakika 30 kabla ya kufa.

Baada ya tukio hilo la ajabu, mumewe alimtoroka na wanawe 6, na maisha yake yakabadilika kabisa, kwani alimtuhumu kwa kufanya mapenzi na mbuzi.

Lakini kisayansi, haiwezi tokea kwamba mtu aliyeshiriki mapenzi na mnyama ana uwezo wa kuzaa mnyama au mnyama kuzaa binadamu.

Kisa cha Alphonsine mpaka sasa kimezalia kuwa kituko ambacho hakiwezi kuelezeka, huku watu katika jamii yake wakiwa wamebaki vinywa wazi baadhi wakihisi huenda alifanyiwa ushirikina.