Ruto apuuzilia mbali madai kwamba waliiba kura 2017

Muhtasari

• Naibu Rais  William  Ruto amepuuzilia mbali madai ya  mwakilishi wa wanawake wa Kaunti ya Kiambu   Sabina Chege kuwa  waliiba kura za uchaguzi wa mwaka wa 2017. 

 

William Ruto
William Ruto
Image: Hisani/DPPS

Naibu Rais  William  Ruto amepuuzilia mbali madai ya  mwakilishi wa wanawake wa Kaunti ya Kiambu   Sabina Chege kuwa  waliiba kura za uchaguzi wa mwaka wa 2017. 

Dkt Ruto  akizungumza katika Kaunti ya Nakuru  ameeleza kuwa wanaoeneza uongo kuwa waliiba kura kwenye uchaguzi uliopita waache kudanganya wakenya na dhana potovu kwani hakuna kura ziliibwa kwenye uchaguzi huo.

"Na mimi nataka niwambie wale wanatukosea heshima kwamba sisi ni wezi wa kura, eti Uhuru Kenyatta na mimi ni wezi wa kura tunawambia waache uchochezi na watuheshimu, sisi tumepigiwa kura na hawa wananchi hakuna kura ya mtu tuliiba, na kama hawa watu wanatumia bangi wapunguze," alisema Ruto.

Ruto ambaye alikuwa ameandamana  na viongozi wa  Kenya Kwanza Alliance(KKA) ; Musalia Mudavadi wa ANC , Moses Wetangula wa Ford-K  na wabunge ambao wanaunga mkono muungano huo.

Ruto aliwauliza wakazi wa  Nakuru kama ni kweli waliwapigia kura.

"Nataka Niwaulize nyinyi watu wa Nakuru, kuna kura ya mtu mliiba? Si mlitupigia kura? Hakuna kura ya mtu tuliiba. Watu wa Azimio waache kutisha watu na maneno ya kuiba kura. Mimi ndiyo nilisimamia maneno ya kura. Hakuna kura ata moja ya mtu Uhuru aliiba".