Wacha kuwadanganya Vijana!- Ruto amwambia Raila

Ruto amemshtumu Raila kwa kuwadanganya Wakenya kuhusu azma yake ya kupunguza gharama ya maisha.

Muhtasari

•Mwanasiasa huyo pia alichukua fursa hiyo kuwahakikishia vijana kuwa pindi atakaposhinda uchaguzi wa Agosti 9,Vijana wote watapata ajira.

•Ruto aliendelea kusema kuwa itakuwa kitu cha aibu kwa wakazi wa Vihiga kaonti kumchagua mtu ambaye tangu utotoni hajawai kushuhudia mateso ambayo watu wa tabaka la chini wanapitia.

Naibu rais na kiongozi wa Kenya Kwanza
Naibu rais na kiongozi wa Kenya Kwanza
Image: William Samoei Ruto (Facebook)

Mgombea wa Urais katika chama cha Kenya Kwanza  Dkt. Wiliam Ruto  amemkashifu vibaya mpizani wake Raila Odinga huku akimshtumu kwa kuwadanganya Wakenya kuhusu juhudi zake za kupunguza gharama ya maisha.

Ruto ambaye alipeleka kampeni zake katika kaunti ya Vihiga tano  aliwatahadharisha wakazi kuhusu ahadi za 'uwongo' za mpinzani wake mkuu katika uchaguzi wa Agosti 9.

''Hawa jamaa wengine na kitendawili hawajawai kulala njaa ata siku moja, hawajui kulala njaa ni nini'' Ruto alisema.

Ruto aliendelea kusema kuwa itakuwa kitu cha aibu kwa wakazi wa Vihiga  kumchagua mtu ambaye tangu utotoni hajawai kushuhudia mateso ambayo watu wa tabaka la chini wanapitia.

'Ata sai tukiongea kuhusu bei ya unga hawaelewi tunasema  nini, sasa ukitegemea mtu mwenye hajawai lala njaa kupunguza bei ya unga, si mtangoja mpaka Yesu arudi'' Ruto alisema.

Mwanasiasa huyo pia alichukua fursa hiyo kuwahakikishia vijana kuwa pindi atakaposhinda uchaguzi wa Agosti watapata ajira.

'' Nyinyi vijana wa Emuhaya  msikubali mtu akuje hapa na hekaya ya Abunwasi ..ooh Vijana tibim ..Vijana tialala..!!!, Sisi tumesema kama Kenya kwanza, tutaweka bilioni mia mbili kwa viwanda zetu hapa nchini ndo tupange ajira ya vijana''  aliongeza.

Aliendelea kukashifu madai ya Raila kuwa Vijana  Wakenya wamekosa elimu na kwa hivyo lengo lake ni kutoa ujinga miongoni mwao.

''Mimi nauliza hapa, watu wa Elungu bado kuna mtu mjinga hapa kweli, si watu wote wamesoma, hawa vijana wamesoma, shida ya hawa vijana sio ujinga, wamesoma wako na shahada, shida yao ni ajira,'' Ruto alisema.