IEBC yafuta kura 10K za Kiambu zilizohesabiwa kimakosa kwa upande wa DP Ruto

Hata hivyo hilo lilirekebishwa baada ya waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo kwa Tume.

Muhtasari

•"Katika Msingi wa Thindigwa ilinaswa kwamba 11 walimpigia kura Odinga badala ya 111. Hilo limesahihishwa katika Fomu C."

•Hapo awali, Tume ilitangaza kuwa DP Ruto wa UDA alikuwa akiongoza katika eneo bunge hilo kwa kura 51,050 dhidi ya 14,860 za Raila licha ya kura zote halali kuwa 56,546.

Kamishna wa IEBC Justus Nyang'aya akiwa Bomas of Kenya mnamo Agosti 12,2022.
Kamishna wa IEBC Justus Nyang'aya akiwa Bomas of Kenya mnamo Agosti 12,2022.
Image: STAR// ENOS TECHE

IEBC Jumamosi iliripoti kura 10,000 zilizotiliwa shaka ambazo zilihesabiwa kimakosa kumuunga mkono Naibu Rais William Ruto kutoka Eneo Bunge la Kiambu Mjini.

Awali, Tume ilitangaza kuwa Naibu Rais Ruto wa UDA alikuwa akiongoza katika eneo bunge hilo kwa kura 51,050 dhidi ya 14,860 za Raila licha ya kura zote halali kuwa 56,546.

David Mwaure na George Wajackoyah walipata kura 318 kila mmoja.

Idadi ya awali iliyotangazwa na Kamishna Justus Nyangaya siku ya Jumamosi ilikuwa kura 10,000 zaidi ya kura zilizopigwa.

Hata hivyo hilo lilirekebishwa baada ya waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo kwa Tume.

Akifanya masahihisho hayo, Nyang'aya alisema Ruto alipata kura 41,050 badala ya kura 51,050 kama ilivyotangazwa awali.

"Katika fomu 34B kulikuwa na makosa, ambayo yalisahihishwa katika fomu 34C, Katika Msingi wa Thindigwa ilinaswa kuwa 11 walimpigia kura Odinga badala ya 111. Hilo limesahihishwa katika Fomu C," alifafanua.

Tafsiri: MOSES SAGWE