STORI ZA GHOST

Stori za Ghost: Mwanamke atema mumewe baada ya chupi za kike saizi kubwa kumliko kupatikana mvunguni

Tangu tukio hilo kutokea mwanadada yule hajaonekana tena pale nyumbani

Muhtasari

•Baada ya mwanamke huyo kurejea kutoka ziara yake, wanandoa hao waliamua kuajiri kijakazi ili awasaidie katika kazi zao za pale nyumbani.

•Kijakazi huyo alifikiria kuwa mwajiri wake alikuwa amepoteza zile chupi mvunguni na kama mfanyakazi mzuri akaamua kumrejeshea.

ghost
ghost
Image: RADIO JAMBO

Ama kweli mizozo haikosi kati ya wawili wapendanao. Kunayo mizozo ambayo ni rahisi kusuluhisha kupitia mazungumzo na vile vile kuna mizozo ambayo hushinikiza wanaopendana kutengana.

Kugundua kuwa huenda mwenzako anatoka nje ya ndoa ni jambo moja ambalo laweza kuvunja ndoa. Kuna ishara nyingi ambazo zinaweza kumfanya mtu kushuku kuwa mwenzake amecheza karata ya nje. Kati ya ishara ambazo hufanya wanawake kushuku mabwana zao ni kukumbana na mavazi ya ndani ya kike ambayo hawayafahamu.

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Stori za Ghost, mtangazaji Ghost amesimulia kisa kimoja kilichotokea jijini Nairobi ambapo mwanamke mmoja ambaye alikuwa ameenda katika ziara zake alirudi na kupata chupi za mwanamke mwingine chini ya kitanda chao cha ndoa.

Ilitokea kwamba mwanamke mmoja kutoka maeneo ya Umoja 1 alifunga safari ya mbali na kumuacha mumewe nyumbani kwa kipindi kisichodhihirishwa.

Baada ya mwanamke huyo kurejea kutoka ziara yake, wanandoa hao waliamua kuajiri kijakazi ili awasaidie katika kazi zao za pale nyumbani.

Alipokuwa kwenye harakati zake za kufanya usafi katika ile nyumba, kijakazi yule alipata chupi zilizokuwa mvunguni na kumpelekea mwanamke mwenye nyumba akidhani kuwa ni zake.

Kijakazi huyo alifikiria kuwa mwajiri wake alikuwa amepoteza zile chupi mvunguni na kama mfanyakazi mzuri akaamua kumrejeshea.

Hata hiyo, mwajiri wake alipozipokea aliona kuwa chupi zile zilikuwa saizi kubwa kuliko anazovaa yeye. Hapo akafahamu kuwa kuna uwezekano bwanake alikuwa ameleta mwanamke mwingine ndani ya nyumba yao.

Huu hapa usimulizi wa Ghost:-

 "Jamaa mke wake kumbe alikuwa ameenda reserve akarejea. Aliporejea nyumbani akakaakaa na akaandika kijakazi mpya. Kijakazi alipokuwa anachokora kwa nyumba akaingia mvunguni. 

Madam alipokuja , kijakazi yule kwa kuwa hakuwa na habari akamwambia 'Madam hizi chupi zako ulisahau mvunguni'. Kijakazi yule hakufahamu kwa kuwa alikuwa mgeni pale.. madam akaangalia chupi akashangaa, ah saizi 22  na mimi ni saizi 8. Hapo akaita bwanake.

Bwana yule alishtuka mkewe alipomuuliza ikawa aje yeye ni saizi 8 na chupi zile ni  saizi 22.. Bibi alimuuliza kwani alileta mwanamke wa aina gani kwa nyumba kwani yeye ni saizi 8" Ghost alisimulia.

Alisema kuwa tangu tukio hilo kutokea mwanadada yule hajaonekana tena pale nyumbani