"Nimeacha mipango ya kando kabisa ata nilienda kanisa Jumapili!" Jamaa ajitetea kwa mkewe

Muhtasari

•Fredrick alieleza kuwa mwanadada ambaye mkewe alimpata akimchezea naye alikuwa mpenzi wake wa zamani aliyetaka warudiane ila yeye hakuwa anamdai.

•Joyce alimwagiza mumewe apige hatua ya kufika kwao nyumbani ili waweze kusuluhisha mzozo wao. 

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Fredrick alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mkewe Joyce Kavole ambaye walikosana hivi majuzi.

Fredrick alisema kuwa mkewe aligura ndoa yao ya mwaka mmoja na kuenda kwao baada ya kumpata na mpango wa kando. 

"Tulikosana kwa mambo madogo madogo kuhusu kutoaminiana. Nilikuwa na mpango wa kando kidogo. Tuliachana na mpango wa kando usiku ambao tulikosana na mke wangu," Joyce alisema.

Fredrick alieleza kuwa mwanadada ambaye mkewe alimpata akimchezea naye alikuwa mpenzi wake wa zamani aliyetaka warudiane ila yeye hakuwa anamdai.

"Mpango wa kando alikuwa wa zamani akanirudia. Sikuwa na hamu naye sana," Alisema.

Joyce alipopigiwa simu alifichua kuwa mumewe alithibitisha kuwa aligura ndoa baada ya kumfumania mumewe na mpango wa kando. Alifichua kuwa Fredrick alikuwa na mazoea ya kutupiana jumbe tamu na wanadada wengine licha ya kuwa kwenye ndoa.

"Itakuwa ngumu. Niligundua alikuwa na mpango wa kando. Alikuwa anachat na watu kwa simu nikaona hayo ni madharau kisha nikaenda kwetu. Alikuwa amezoea. Sijui kama umeacha hiyo tabia mbaya ambayo ulikuwa nayo,"  Joyce Alisema.

Fredrick alijitetea kwa mkewe huku akisisitiza kuwa tayari ameacha tabia ya kutoka nje ya ndoa. Alimhakikishia mkewe kuwa anampenda sana na kumwomba arudi.

"Nimeacha kabisa ata nilienda kanisa Sunday. Nimebadilika kabisa. Nimeacha hayo maneno. Naomba urudi," Joyce alisema.

Joyce alimwagiza mumewe apige hatua ya kufika kwao nyumbani ili waweze kusuluhisha mzozo wao. Alimhakikishia Fredrick kuwa angekubali kumsamehe iwapo atachukua hatua ya kumuendea nyumbani kwao.