'Hakuna dem alidoz na Eric Omondi ,'Mmoja wa washiriki aweka mambo wazi

Muhtasari
  • Mmoja wa washiriki a wife material asema Eric hakulala na msichana yeyote
  • Hii ni baada ya mwanasosholaiti Shakilla kudai kwamba ana ujauzito wake mchekeshaji huyo

Mmoja wa washiriki wa kipindi cha 'wife material'cha mchekeshaji Eric Omondi ameweka mambo wazi na kusema kwamba hamna msichana yeyote alilala na Omondi.

Mbali na hayo alisema kwamba mchekeshaji huyo aliwapa heshima nyingi sana.

Pia alifichua kuwa alikuwa anataka tu kujifurahisha kupitia kipindi hicho na wala hakuwa anataka kuolewa na mchekeshaji huyo.

 

Shila kutoka Kitale alidai kwamba yeye ni mrembo na ananggoja mumewe na hangeenda kwenye televisheni kutafuta mume.

"Hizo rumors etu tulidoze na Eric, no no! Hakuna Dem alidoze na Eric, aliturespect he was a good boss na mimi nilienjoy going to these places, Mombasa and Nanyuki. It was the best experience ever

Mimi ni Dem nina dignity zangu na nilienda io show kuhave fun not that I was looking for a husband

Mimi ni Dem mrembo nitapata mwanaume huku nje na maybe Niko naye. Mimi nilikuwa ninawafurahisha tu." Shila Aliongea.

Ni kipindi ambacho kilipeperushwa kwenye youtube huku Eric sku ya jumanne 23 Desemba akipata mkewe ambaye alichaguliwa na wakenya.

Usemi wake Shila unajiri saa chache baada ya mwanasosholaiti Shakilla kudai kwamba ana ujauzito wake Eric.