DRAMA ZA ERICO

Erico alaumu mgombeaji kwa kusitishwa kwa 'Wife Material'

Mgombeaji @gigy_money_og kutoka Tanzania atishia kutoboa siri kuhusu mbona onyesho hilo limesitishwa

Muhtasari

•Wanamitandao wengi wameshuku kuwa kunalo jambo Erico anaficha

•Mgombeaji @gigy_money_og kutoka Tanzania atishia kutoboa siri kuhusu mbona onyesho hilo limesitishwa 

eric omondi na wagombeaji
eric omondi na wagombeaji
Image: Hisani

Mcheshi Eric Omondi ametangaza kusitishwa kwa kipindi cha pili cha ‘Wife material’ kwa kile alichosema ni kupotoka kwa mgombeaji mmoja na kukosa kudhibitika kwa hali baina ya wagombeaji.

Onyesho hilo ambalo lilikuwa limetangazwa kuanza tarehe 24 Mei halitafanyika tena hata baada ya wagombeaji zaidi ya kumi kutoka nchi mbalimbali Afrika Mashariki kuzinduliwa.

Nia ya onyesho la Wife Material ni kutumbuiza watu na zaidi kabisa kuwafanya wagombeaji kuwa na starehe, kujiskia salama na kuwa na wakati wa kufana wanaposhindana. Kwa bahati mbaya, mgombeaji mmoja alipotoka na juhudi za kudhibiti hali katika nyumba ile hazikufua dafu” Omondi alitangaza kupitia chapisho kwenye akaunti yake ya Instagram.

Hata hivyo, mcheshi huyo ameeleza kuwa atarejea na kipindi cha pili cha onyesho hilo.

Mmoja wa wagombeaji kwa jina @gigy_money_og kutoka Tanzania alimjibu Omondi kwa hasira akionyesha kutoridhika kwake na matukio hayo huku akimtishia kuwa angejuta baada yake kuambia watu ukweli wa mbona onyesho halitaendelea.

Kwa hivyo Eric, uliniita hapa nitukanwe ju unapata dili na kuwarekodi watu bila kujua unatufanya sisi vituko. Unajua kuwa utajuta haya na hutawasahau mabibi zako.. una dada kweli?? Nikiamua kuambia watu kwa nini onyesho haliendelei utanilaumu” Gigy aliandika.

ujumbe wa gigy
ujumbe wa gigy
Image: Hisani

Wanamitandao wengi wamedai kuwa kunalo jambo Eric anaficha huku wakimuomba Gigy kutoboa siri.