Video ya binti mdogo akiita jina la babake juu ya kaburi lake yaliza wanamitandao

Binti huyo mdogo chini ya miaka kumi alidaiwa kuenda kaburini hapo kila baada ya wiki 2.

Muhtasari

• Msichana huyo alikuwa na mazoea ya kwenda kumwona marehemu babake kila baada ya wiki mbili.

Watumizi wa mitandao ya kijamii walihuzunika baada ya  video ya msichana mdogo akiongea kando na kaburi la marehemu babake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Video hiyo ambayo ilipakiwa kwenye mtandao wa Tiktok, ilimwonyesha mwanadada huyo mchanga akiwa ameinama kaburini huku akimwita babake akiwa na matumaini pengine angeitika.

Kwa huzuni nyingi msichana huyo alirejea kwa mlezi wake baada ya kumwita babake mara kadhaa.

"Hello papa!  hello papa!'' msichana huyo aliita mara kadhaa bila jibu.

Kwenye chapisho ambalo liliambatanishwa na video, ilidhihirisha kuwa msichana huyo amekuwa na mazoea ya kufika kaburini baada ya wiki mbili na kumsalimia babake aliyekufa Novemba 8, 2021.

"Amekuwa akiomba kumwona babake baada ya kila wiki mbili"  Video hiyo ilieleza.

Kwenye chapisho lingine kwenye video ilisema "Daima amekuwa akimkumbuka babake."

Wanamitandao ambao mioyo yao ilikuwa imeyeyushwa na kitendo cha msichana walituma maelfu ya jumbe kuomboleza pamoja na mtoto huyo. Wanamitandao walisema kuwa mapezi alionayo kwa babake hayawezi pimika wala kutambilika licha ya kuwa hatawai kumwona babake bali tu kwa picha.

Mojalefa alisema, ''Nahisi babake alikuwa akitabasamu tu penye ako. Usichoke kumpeleleka mtoto huyo kumsalimia babake.''

Lerato alisema huku akipiga dua, ''Video inagusa moyo sana. Nawaombea Mwenyezi Mungu awe nanyi siku zote za maisha yenu."

Noxee09, ''Video imenigusa moyo. siwezi waza mtoto wangu akipitia kama haya.''

Mbali na hayo wanamitandao walionekana kumpongeza mlezi wa mtoto huyo kwa kufanya jambo la busara la kumpeleka kwenye kaburi mwa babake ili asije akapatwa na maswali mengi kuhusu aliko baba yake anapokuwa.