Bahati amzawadi mkewe Diana Marua nyumba kifahari

Muhtasari

• Bahati amemtunuku mkewe, Diana Marua   nyumba ya kifahari kama zawadi ya kusherehekea siku ya wapendanao

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Msanii Kevin Bahati amemtunuku mkewe, Diana Marua   nyumba ya kifahari kama zawadi ya kusherehekea siku ya wapendanao.

Kupitia ukurusa wa Diana, alieleza kuwa mumewe alimtunuku chumba hicho siku ya wapendanao kama zawadi ya kuwa mvumilivu kwenye ndoa.

Mpenzi wangu alinipandisha gari na kunishtua na nyumba mpya, Asante Mungu kwa kuwa mvumilivu, Mfalme wangu, Bahati nimezidiwa na furaha,bado sina maneno ya kuelezea jinsi ninavyohisi,”alisema Diana Marua.

Hii imewadia baada ya mcheshi Alex Mathenge kuwa na shaka ya zawadi ambazo Diana hupewa na mumewe akihisi kama ni kiki tu wasanii hao wanatengeneza kuhakikisha wanatambulika.

Diana Marua amejitosa kwenye tasnia ya muziki ambapo mwaka huu ametoa kibao kimoja.

Ikumbukwe ni wiki jana ambapo Bahati alimzawadi  mkewe gari jipya, kitendo ambacho kilifanya Diana kutiririkwa na machozi ya furaha njia mbili na kudhihirisha furaha alikuwa nayo kwa  mumewe.