Rayvanny akiwasha Ufaransa wakati Diamond anazindua EP

Muhtasari

• Rayvanny alitia 'performance moja ya nguvu jijini Paris usiku wa kuamkia Ijumaa akiwa jukwaani na gwiji wa Columbia Maluma.

Rayvanny
Image: Instagram

Msanii Rayvanny ambaye ametokea rekodi lebo ya Wasafi na sasa hivi ni tajiri mwenye lebo yake ya Next Level Music anazidi kuzikwea ngazi za kimuziki duniani na wengi wanahisi jitihada zake kimuziki huenda zinamzolea tuzo nyingi za kimataifa kama Grammy, baada ya kutia kibindoni ile ya BET miaka miwili iliyopita.

Alhamis usiku wakati ‘baba’ yake wa muziki Diamond Platnumz anazindua EP yake ya FOA mabayo ni ya kwanza kabisa katika safari yake ndefu ya muziki nchini Tanzania, Rayvanny alikuwa jijini Paris, Ufaransac akipiga mishe la nguvu kabisa.

Baadae Rayvanny alipakia video akiwa kwenye jukwaa moja na gwiji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Columbia, Maluma.

Rayvanny anaonekana na kusikika pia akimsifia sana Maluma kwa ueledi wake katika lugha ya kizungu na kuwakosa kwa vitendo wale wanaosema kwamba wasanii kutoka Afrika mashariki na haswa Tanzania hawana uelewa wa kihivyo katika lugha hiyo la Malkia wa Uingereza.

Msanii huyo mkali wa ‘Tetema’ anasikika akiutaka umati kwenye ukumbi huo kumpigia makofi mara kumi nguli wa kibao cha ‘Hawai’, Maluma.

Watu wengi wamemsherehekea Rayvanny na kusema kwamba anaenda mbali ambapo wengi wanahisi sasa amekua kuteuliwa kuwania tuzo zenye maskio marefu kama Grammy kwani mchango wake katika sanaa ya muziki na haswa Afrika mashariki umekuwa mkubwa sana.

Je, unahisi mchango wa Rayvanny katika muziki umefikia viwango vya kuteuliwa kuwaia tuzo za Grammy?