Zari aweka wazi chanzo cha mapato yake

Zari alifichua baadhi ya kazi anazofanya sasa ili kumudu familia yake

Muhtasari

• Aliwaonya watu kuhusu walaghai wanaotumia jina lake kwa kusema kuwa yeye hufanya biashara mtandaoni ikiwemo biashara ya mtandaoni ya forex.

Zari Hassan

Mfanyibiashara Zari Hassan aliweka wazi asili ya mapato yake baada ya visa kutokea ambapo watu wameibiwa kwa kutumia jina lake.

Zari alisema kuwa kazi anayofanya ni ya kufanya vipindi vya uhalisia na matokeo kwenye runinga miongoni mwa kazi zingine.

Mama huyo wa watoto watano alisema kuwa yeye ni mwenye vyuo vikuu kadhaa huko Afrika Kusini na kuwa hauzi nguo zozote zile wala bidha za wanawake za urembo mtandaoni.

Aliwaonya watu kuhusu walaghai wanaotumia jina lake kwa kusema kuwa yeye hufanya biashara mtandaoni ikiwemo biashara ya mtandaoni ya forex.

Asili ya tatu ya mapato ya Zari ambayo alitaja ni kuwa yeye ni balozi wa makampuni mengi  na bidhaa zingine.

Zari alisema pia kuwa amejikita kwenye elimu na kufunza watu kimaarifa kama kazi yake nyingine ili aweze kujikimu yeye na watoto wake.

Alieleza kuwa walaghai wanatumia jina lake, picha zake, magari yake na hata kuwa na akaunti feki ili kulaghai na kuwaibia pesa watu ambao hawajui akaunti yake ya ukweli.

Aliwaonya mashabiki wake kuhusu walaghai hao na kuweka wazi kazi anazofanya ili watu wasiibiwe tena.

"Mnaibiwa huko nje kutumia akaunti zilizo na jina langu kisha mkishaibiwa mnanitafuta kutumia akaunti yangu kunilalamikia kuwa mnataka pesa zenu, pesa gani?" Zari aliwafokea watu hao.

Alisema kuwa hajui kuhusu biashara zozote ambazo ziko mtandaoni na jina lake ama picha yake na kuwa kitu chochote watakachoona kwenye mitandao na vitu hivyo ni bandia na haijatoka kwake.