Bei ya mbolea 50kg kuteremka kutoka 6500 hadi 3500 kuanzia wiki kesho - rais Ruto

Katika hotuba yake kama raia, Ruto alirudia baadhi ya ahadi zake kwa Wakenya na kusema atajitahidi uzitekeleza.

Muhtasari

• Mkakati wetu wa kupunguza gharama ya maisha unalenga kuwawezesha wazalishaji - Ruto

Rais wa tano Ruto na baadhi ya ahadi zake siku ya kuapishwa
Rais wa tano Ruto na baadhi ya ahadi zake siku ya kuapishwa
Image: Facebook//William Ruto

Baada ya Ruto kuapishwa rasmi kama rais, katika hotuba yake ya kwanza, kiongozi huyo alitoa ahadi sufufu kwa Wananchi.

 Katika moja ya ahadi zake, rais Ruto alisema kwamba bei ya mbolea ambayo kwa sasa iko zaidi ya elfu 6 kwa gunia ya kilo 50, bei yake itashuka kutoka 6500 hadi shilingi 3500 kuanzia wiki kesho.

"Mkakati wetu wa kupunguza gharama ya maisha unalenga kuwawezesha wazalishaji. Utabiri wa uzalishaji wa mahindi mwaka huu uko chini ya magunia milioni 30 dhidi ya uzalishaji wa kawaida wa magunia milioni 40. Sababu kuu ni kushuka ni gharama kubwa ya pembejeo za kilimo," Ruto alisema.

"Kwa mvua hizo fupi, tumefanya mipango ya kufanya mifuko milioni 1.4 ya mbolea ipatikane kwa KSh 3,500 kwa mfuko wa kilo 50 kutoka KSh 6,500 za sasa," aliongeza rais.

Akionekana kuzungumzia zaidi maisha ya watu wapambanaji wenye kipato cha kadri, Ruto alisisitiza kwamba atarahisisha maisha kama ilivyokuwa ahadi yake kweney manifesto ya Kenya Kwanza.

Vile vile, Ruto alisema atawateuwa majaji wote waliopendekezwa na idara ya mahakama ili kuanza kuhudumu mara moja bila kusita.

Ruto alisema shughuli hiyo itafanyika jioni ya leo na kesho Septemba 14 atasimamia shughuli ya kuapishwa kwa majaji hao ambao walitemwa nje ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta wakati wa kuwateua majaji kutoka kwa orodha aliyokabidhiwa na idara ya mahakama.

Ruto alisisitiza uhuru wake na heshima kwa idara ya mahakama na kusema kwamab atazidi kuwapa ushirikiano unaofaa ili kuendeleza kutatua masuala mbali mbali wakiwa na uhuru kulingana na katiba ya mwaka 2010.

“Utawala wangu utaongeza mgao wa bajeti kwa Idara ya Mahakama kwa nyongeza ya bilioni KSh 3 kila mwaka kwa miaka mitano ijayo ili kuunga mkono uwekaji haki kutoka chini kwenda juu kwa kuongeza idadi ya mahakama ndogo za madai kutoka 25 hadi 100 za sasa,” rais Ruto alisema.