Raila ashindwa katika kituo cha kupigia kura cha Mutomo cha Uhuru Kenyatta

Matokeo yote kutoka kwa mikondo minne ndani ya shule yalikuwa yamepakiwa.

Muhtasari

• Katika fomu hizo, Raila alipata kura 464 huku mpinzani wake DP William Ruto akipata kura 983.

• Kiongozi wa chama cha Roots George Wajackoyah alikuwa na kura 9 huku chama cha Agano Waihiga Mwaure kikiwa na kura 4.

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Old Kibera mnamo Agosti 9, 2022.
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Old Kibera mnamo Agosti 9, 2022.
Image: THE STAR//ENOS TECHE

Mgombea urais wa Azimio Raila Odinga alishindwa katika kituo cha kupigia kura cha Rais Uhuru Kenyatta, ambacho ni shule ya Msingi ya Mutomo huko Gatundu.

Kulingana na kfomu za 34A zilizopakiwa kwenye tovuti ya IEBC, matokeo yote kutoka kwa mikondo minne shuleni yalikuwa yamepakiwa.

Katika fomu hizo, Raila alipata kura 464 huku mpinzani wake Naibu Naibu William Ruto akipata kura 983.

Mgombea urais wa chama cha Roots George Wajackoyah alikuwa na kura 9 huku chama cha Agano chake Waihiga Mwaure kikiwa na kura 4.

Kulikuwa na idadi ndogo ya wapiga kura katika kituo cha Mutomo huko Gatundu Kusini, kituo ambacho Jumanne asubuhi rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta alipoga kura yake pamoja na mkewe Mama Margret kenyatta.

Mgombea ubunge wa Gatundu Kusini Peter Kibathi alisema huenda hali mbaya ya anga ilichangia idadi hiyo ndogo.

Alisema Wakenya wanapaswa kujitokeza na kuwapigia kura viongozi ambao watabadilisha maisha yao.

“Ningependa kupongeza IEBC kwa kufanya kazi nzuri lakini idadi ya wapiga kura ni ndogo sana ikilinganishwa na chaguzi zilizopita,” akasema.

Taarifa zingine pia zilikuwa zinasema kwamba Raila alipaka kura chache katika kituo cha kupoga kura cha mgombea mwenza wake Martha Karua huku mshindani wake William Ruto akiwa na kura nyingi katika kituo hicho cha Mugumo kaunti ya Kirinyaga.