Embu: Mwanaume aliyejifanya ajenti wa Raila akamatwa na fomu za matokeo za IEBC

Ajenti wa mgombea urais wa Azimio la Umoja ambaye amekuwa hapo siku zote alisema hamfahamu mtu huyo.

Muhtasari

• Mtu huyo baadaye alikamatwa na polisi waliokuwa wakisimamia kituo hicho.

Mwanaume (kulia) anayeshutumiwa kwa kumiliki fomu za matokeo za IEBC kinyume cha sheria
Mwanaume (kulia) anayeshutumiwa kwa kumiliki fomu za matokeo za IEBC kinyume cha sheria

Ghasia zilizuka katika kituo cha kuhesabia kura cha Runyenjes huko Embu baada ya mwanamume aliyejifanya ajenti wa Raila Odinga kunaswa akiwa na fomu 34B na 37B kwenye gari lake nje ya ukumbi huo wa kuhesabika kura.

Haya yalijiri baada ya maajenti wa wagombea ugavana kuzua tafrani ukumbini baada ya kubainika kuwa fomu hizo hazipo.

Mtu huyo ambaye hakutambuliwa alisema alikuwa ametumwa na aliyekuwa PS Cyrus Njiru na mwenyekiti wa Azimio la Umoja katika Kaunti ya Embu kuwa ajenti wa urais wa Azimio la Umoja.

Lakini ajenti wa mgombea urais wa Azimio la Umoja ambaye amekuwa hapo siku zote alisema hamfahamu mtu huyo.

‘Tapeli’ huyo alilazimika kuwaeleza wananchi waliokuwa wamekusanyika ukumbini hapo alipopata fomu hizo na kusema alizipata kwa Msimamizi wa Uchaguzi Pamela Karimi.

Mtu huyo baadaye alikamatwa na polisi waliokuwa wakisimamia kituo hicho.

Baada ya kukamatwa, maajenti mgombeaji wa ugavana wa Embu, Lenny Kivuti walitoka nje ya kituo cha kujumlisha kura wakipinga matokeo hata kabla ya kutia sahihi fomu hizo.

Naibu Msimamizi wa Uchaguzi George Miriti aliwaambia maajenti hao kwamba fomu hizo zitawasilishwa nazo au bila wao.

Mawakala wa gavana Cecily Mbarire, hata hivyo, walitia saini fomu hizo na kuelekea Kangaru kwa kujumlisha mwisho.

Chama cha UDA cha Mbarire and Development Empowerment Party (Mbus) Kivuti kiko kwenye vita vikali kumtafuta gavana wa Embu.

Wawaniaji wengine wawili wa kiti hicho ni Emilio Kathuri wa Jubilee na Njagi Kumantha wa DP. Kura za mwisho za maoni zinaonyesha ushindani upo kati ya Kivuti na Mbariri.

Embu ina wapiga kura 334,302 waliojiandikisha, kulingana na rejista ya wapiga kura iliyotangazwa kwenye gazeti la serikali.

Manyatta ana wapiga kura 106,588, akifuatiwa na Runyenjes 95,326, Mbeere Kusini 77,264 na Mbeere Kaskazini 55,124.

 

Tafsiri: MOSES SAGWE