Mgombea huru Mwadime ambwaga Samboja wa Jubilee na kushinda ugavana Taita Taveta

Aliyekuwa gavana John Mruttu (UDA) alimaliza wa tatu kwa kura 13,865 huku seneta wa zamani Dan Mwazo (Wiper) akipata kura 11,543 katika nafasi ya nne.

Muhtasari

• Mwadime anakuwa gavana wa pili kuchaguliwa kwa tiketi huru baada ya Kawira Mwangaza wa Meru ambaye alimshinda mwanasiasa mkongwe Kiraitu Murungi.

Gavana mteule wa Taita Taveta Andrew Mwadime na naibu wake Christine Kilalo wakishikilia cheti chao katika Chuo Kikuu cha Taita Taveta Jumamosi
Gavana mteule wa Taita Taveta Andrew Mwadime na naibu wake Christine Kilalo wakishikilia cheti chao katika Chuo Kikuu cha Taita Taveta Jumamosi
Image: STAR//SOLOMON MUINGI

Mbunge wa Mwatate anayeondoka Andrew Mwadime ameshinda kiti cha ugavana kaunti ya Taita Taveta. Mwadime, mgombeaji wa kujitegemea alitangazwa mshindi na afisa wa uchaguzi wa Kaunti wa IEBC Esha Mohammed Jumamosi asubuhi.

Wakujaa, kama anavyotajwa na wafuasi wake alimshinda gavana aliyemaliza muda wake Granton Samboja kwa kura 49,901 na kushinda kiti hicho. Samboja wa chama cha Jubilee aliibuka wa pili kwa kura 23,703.

Aliyekuwa gavana John Mruttu (UDA) alimaliza wa tatu kwa kura 13,865 huku seneta wa zamani Dan Mwazo (Wiper) akipata kura 11,543 katika nafasi ya nne.

Mwadime anakuwa gavana wa pili kuchaguliwa kwa tiketi huru baada ya Kawira Mwangaza wa Meru ambaye alimshinda mwanasiasa mkongwe Kiraitu Murungi.

Shindano hilo lililojaa watu wengi lilikuwa limewahoji washiriki 13. Waliojumuisha wapya wa kisiasa kama Stephen Mwakesi (PEP), mwanahabari Patience Nyange (Narc), George Mwandembo (DAP), Prof Agnes Mwang'ombe (ANC), Godino Mwasaru (Kujitegemea), Onsemus Mwinzi (Kujitegemea), Tom Mwakwida, (ODM), Faustin Mghendi (TSP) na Francis Mwaita wa Safina.

Gavana huyo mteule katika mahojiano alisema ataweka kipaumbele katika kufufua uchumi wa eneo hilo na kuwasaidia wakazi kuongeza uzalishaji wa kilimo.

"Timu yangu ina orodha ndefu ya vipaumbele lakini tutashughulikia kupambana na njaa na kufufua uchumi," alisema.

Alisema atawakutanisha viongozi wengine wote ili kuweka mikakati ya namna ya kuleta maendeleo katika mkoa huo.

Hapo awali, wafuasi wa Mwadime walikuwa wamepinga kuchelewa kutangazwa kwa matokeo. Walisema kuwa bodi ya uchaguzi imechukua zaidi ya saa 73 kujumlisha na kutangaza matokeo licha ya idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza kupiga kura.

"Kaunti zingine zilizo na mamia ya kura kujumlisha tayari zimetangaza matokeo huku tungali hapa tukijumlisha chini ya kura mia moja," Harrison Kamwana alisema.

Alisema kuchelewa kumesababisha wasiwasi miongoni mwa wafuasi.

 

Tafsiri: MOSES SAGWE