PS Susan Auma anamtafuta mchuuzi ambaye Kanjo walimwaga njugu karanga zake

Katibu Susan hata hivyo alimtaka Gavana Sakaja kuweka mazingira bora ya biashara ndogo ndogo jijini ili kuepuka visa kama hivi.

Muhtasari

• Kupitia ukurasa wake wa X Auma aliwakosoa maafisa hao na kumtaka gavana wa Nairobi Johnson Sakaja kuwachukulia hatua za kisheria.

•"Wapendwa wazalendo,ninawasihi mnisaidie kumpata mchuuzi huyu ambaye juhudi na riziki yake zimeathirika pakubwa,"

Image: SCREENGRAB

katibu wa kudumu wa wizara ya Ushirika na biashara ndogo ndogo Susan Auma,amewataka wakenya kumsaidia kumtafuta kijana ambaye alidhalilishwa na afisa wa Kanjo jijini Nairobi.

Kupitia ukurasa wake wa X Auma aliwakosoa maafisa hao na kumtaka gavana wa Nairobi Johnson Sakaja kuwachukulia hatua za kisheria.

"Wapendwa wazalendo,ninawasihi mnisaidie kumpata mchuuzi huyu ambaye juhudi na riziki ake imeathirika pakubwa,"aliandika.

Katibu Susan hata hivyo alimtaka Gavana Sakaja kuweka mazingira bora ya biashara ndogo ndogo jijini ili kuepuka visa kama hivi.

"Serikali ya Kaunti ya Nairobi inayoheshimika inayoongozwa na Gavana sakaja ,naomba kwa dhati kurasimishwa na kuunganishwa kwa biashara ndogo ndogo ,pamoja na kuweka mazingira bora kwa biuashara hizo,"aliongeza.

Watu  mbali mbali wametoa hisia zao wakikashifu vikali kitendo hicho cha unyama,huku baadhi wakidai kuwa tabia ya maafisa hao sasa imezidi na kumtaka Gavana wa Nairobi kuchukulia hatua kiendo hicho.

VDJ Jones alimkshifu afisa huyo akisema: “ Hawa makanjo huona wamefika sana. Laana ya machozi itakufuwata hadi kitandani mwako, iko siku.”

“Huyu Kanjo vile amenona nikukula hongo ata haezi hurumia mvulana,” soma maoni mengine.

Hata hivyo baadhi wamejitokeza na kujitolea kumpiga kijana huyo jeki ili aendelee na kujikimu kimaisha

Mchekeshaji Eric Omondi ameeleza nia yake ya kutaka kutoa msaada kwa kijana huyo.

Omondi amesema wazi kuwa ana nia ya kutaka kumpiga kijana huyo jeki huku akiwataka wale ambao wana uwezo wa kumfikia kijana huyo kumwelekeza kwake.

Mcheshi huyo aliyegeuka kuwa mwanaharakati amekuwa akiweka tabasamu kwenye nyuso za watu katika miezi michache iliyopita.