Polisi Waanzisha uchunguzi Kwale Kufuatia Kutoweka kwa Fomu 35A za Kura

Maafisa wa DCI wanachunguza suala hilo.

Muhtasari

• “Msimamo wa kisheria hapa ni kutumia jumla ya wapiga kura waliojiandikisha katika kituo cha Kifyonzo" - Afisa huyo wa IEBC alisema.

Afisa msimamizi wa kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Kifyonzo alikosea fomu ya MNA (35A) jambo ambalo limesababisha kucheleweshwa kutangaza matokeo katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale.
Afisa msimamizi wa kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Kifyonzo alikosea fomu ya MNA (35A) jambo ambalo limesababisha kucheleweshwa kutangaza matokeo katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale.

Polisi katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale wanachunguza kisa ambapo afisa msimamizi alikosa kutoa fomu 35A.

Afisa wa upigaji kura wa shule ya msingi ya Kifyonzo alisema kuwa aligundua kuwa fomu haipo baada ya kufika katika kituo cha kujumlisha kura.

Alielekezwa kuangalia katika masanduku yote ya kura ambayo yalifunguliwa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi na maajenti wakuu lakini hakuna kilichopatikana.

"Nina Afisa Mkuu wa Polisi ambaye alipoteza fomu ambazo tulipaswa kutumika kujumlisha matokeo, suala ambalo halina uwezo wangu na sasa polisi wanapaswa kuhusika," afisa wa mkuu Joseph Mwafondo alisema.

Mwafondo alisema kuwa watalitatua suala hilo kwa amani.

“Msimamo wa kisheria hapa ni kutumia jumla ya wapiga kura waliojiandikisha katika kituo cha Kifyonzo kuamua jinsi tutakavyogawa kura kati ya wabunge 10 kulingana na jinsi wamefanya katika vituo vingine 236,” alisema.

“Iwapo kuna mtu atahisi hajaridhishwa na utaratibu huo, anaruhusiwa kupeleka suala hilo mahakamani,” aliongeza.

Afisa wa kituo cha kuhesabu kura cha Kinango Fredrick Ombaka alisema kuwa bado hawajui ni wakati gani mkanganyiko huo ulitokea lakini maafisa wa DCI wanachunguza suala hilo.

“Tuko katika mawasiliano na IEBC kwa mashauriano lakini maafisa wa DCI ndio wanastahili kufanya uchunguzi,” akasema.

Kituo cha kupigia kura kina wapiga kura 453.

Haya yanaripotiwa saa chache baada ya afisa msimamizi wa kituo cha kupiga kura cha Old Kibra ambapo Raila alipiga kura kusema kwamba fomu 34A zilipotea pia chini ya ulinzi wake.