• “Ni lazima tumpe sifa William Ruto kwa mafanikio haya yote mezani na timu yake" - Kioni.
Mbunge anayeondoka wa Ndaragua Jeremiah Kioni ambaye pia anajiongeza kama Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee, baada ya kupoteza kiti chake sasa amesema wao kama Jubilee walikuwa wanapuuza ushawishi wa Naibu Rais William Ruto katika eneo la Mlima Kenya.
Kioni ambaye alikuwa anawania kuwa mbunge wa Ndaragua kwa mara ya tatu kupitia tikiti ya chama cha Jubilee, alikipokea kichapo cha mbwa msikitini kutoka kwa George Gachagua ambaye alikuwa anagombea kwa tikiti ya chama cha UDA.
Akizungumza katika kituo kimoja cha runinga cha humu nchini Ijumaa jioni, Kioni alisema kwamba eneo pana la Mlima Kenya lilikuwa limedunisha muungano wa Kenya Kwanza na haswa UDA cha William Ruto ambacho kiliibukiwa kunyakua nyadhifa nyingi katika uchaguzi ambao umekamilika hivi majuzi huku wengi wa waliokuwa wakiwagia kwa chama cha Jubilee wakioneshwa kivumbi cha karne.
“Ni lazima tumpe sifa William Ruto kwa mafanikio haya yote mezani na timu yake, kuhusu jinsi gani tunafaidika na matukio haya yote?… Anachukua hii na kuitumia kwa njia hiyo…ni mchezo wa kufukuza, na pia nikubali kwamba tulipuuza jinsi watu wetu walikuwa wanatumiwa,” Kioni alisema katika mahojiano.
Wengine ambao walikuwa wakiwania kwa chama cha Jubilee na kubwagwa na UDA eneo la Mlima Kenya ni pamoja na mbunge wa Kipipiri Amos Kimunya, mbunge wa Kieni Kanini Kega, mbunge wa Nyeri Town Ngunjiri Wambugu miongoni mwa wanasiasa wengi ambao wanazidi kuungulia kudhailishwa na kuchachawizwa na UDA chake William Ruto.